KUNA UWEZEKANO WA KUPANGILIA KUPATA MTOTO WA KIKE/KIUME?
Kwanza tufahamu kuwa kuna aina mbili za mbegu amabzo ndio matokeo ya kupatikana kwa mtoto wa kike au kiume, aina za mbegu hizo ni XY na XX. XY ni mwanaume na XX ni mwanamke. Endapo mwanaume atatoa mbegu X na kuungana na ya mwanamke X matokeo yake ni mtoto wa kike.na kuungana kwa mbegu Y ya mwanaume na ile ya mwanamke X basi matokeo yake ni mtoto wa kiume(XY)
Mbegu X zina sifa ya kuwa na spidi ndogo dhidi ya Y lakini zinauwezo wa kuhimiri hali ya kimazingira(asidiki) iliyopo katika uke wa mwanamke katika safari yake na hivyo kuifanya kuwa na uwezo wa kuishi muda mrefu zaidi ya Y. Mbegu za Y zina spidi kubwa zaidi ya mbegu X lakini haina uwezo mkubwa wa kuhimiri hali ya asidiki iliyopo katika uke wa mwanamke.
kwa maana hiyo ili uweze kupangilia kumpata mtoto wa kike au wa kiume ni vizuri kufatiliza vizuri siku za mwenzi za mwanamke(menstruation cycle). Kawaida ya mwanamke mzunguko wake ni siku 28 na siku inayokadiriwa yai kushuka ni siku ya 14 kabla ya hedhi inayofata.
Wanawake wengi huwa wanaviashiria ya kujua kama wapo katika siku za kushuka kwa yai na baadhi huwa inapita pasi na kufahamu.Miongoni mwa dalili hizo ni kutokwa na majimaji mazito yenye kuvutika misili ya yai bichi katika uke na kupanda kwa joto mwili. kwa wengine wanaweza kujua kwa kutumia kikokotoo cha uchevushaji(ovulution calculator).
Vitu vya kufanya katika siku hizi
Uwe na kipimio cha jotoridi(Thermometer) ambayo unaweza kupata katika maduka ya dawa. Utatumia kwa ajili ya utambuzi wa kujua siku ya yai kushuka. Muda wa kupima ni kila siku asubuhi,siku utakayoona jotomwili limezidi kawaida ujue ndio dalili ya kushuka kwa yai
Jizuie kula vyakula vinavyoongeza PH, kama vile; maziwa, na kula vyakula vinavyopunguza PH, mfano maji, mbogamboga, matunda.....Hii itasaidia kupunguza kiwango cha asidi kinachopatikana katika sehemu ya uke na kuwezesha mbegu Y kuweza kuhimiri na hatimaye kufikia yai.(hii kwa wale wanaotaka watoto wa kiume)
Mwanaume aongeze wingi wa manii, Namna ya kuongeza ni moja kwa kujizuia kutotoa manii (kwa kujichua au tendo la ndoa) kwa siku 5 au zaidi. Kula vyakula vinavyochochea uzalishaji wa manii kama karanga, nazi, mihogo mibichi nk.Usivae nguo zinazobana sehemu zako za uume na korodani, Kawaida semen huzalishwa kwa wingi katika mazingira ya ubaridi hiyvo kwa kujizuia kuvaa nguo za kubana utapunguza joto na kuzifanya manii/semeni zizalishwe kwa wingi.
Wakati wa tendo la ndoa hakikisha mwanamke anafikia kileleni kabla yako, Mwanamke anapofikia kileleni huwa anazalisha majimaji kwa wingi katika sehemu zake za kike ambayo husaidia kupunguza usumu(asidi) dhidi ya mbegu. Mbegu ya Y ndio huwasiliwa zaidi, kwa maana hiyo kwa muhitaji wa mtoto wa kiume yampasa awe makini
Wakati wa tendo la ndoa ni vizuri kutumia Style ambayo itaruhusu kwa urahisi mbegu kupenya (Penetration Style), itapunguza safari ya mbegu na kupunguza upingamizi (asidiki )
SUMMARY
Kama wenza wana malengo ya kupata mtoto wa kiume basi inawapasa wafanye tendo la ndoa siku mbili au tatu kabla ya yai kushuka, kwa kuwa mbegu y ina spidi zaidi ya X itaifanya kufika mapema na kuungana na chembe X iliyobaki kwa mwanamke.
Na kwa wahitaji wa watoto wa kike itawabidi wafanye siku nyingi zaidi, kwa siku ya 9, 10 na 11 (kwa wanawake wenye mzunguko wa siku 28). Kwa tabia ya mbegu X kuwa na uhai mrefu itaiwezesha kufikia mbegu X iliyopo kwa mwanamke na kuungana kutengeneza XX.
Muhimu
wanawake wenye mizunguko ya siku 28 makadirio ya siku za kushuka kwa yai ni siku ya 14, na wenye mizunguko ya siku 21 yai hushuka siku ya 10 na wenye mizunguko mirefu wa siku 36 yai hushuka siku ya 18.
*****Kumbuka kuwa Mola muumba wa mbingu na Ardhi ndiye mkadiriaji wa kupata mtoto wa kiume au wa kike*****