UGONJWA WA HERNIA



Ugonjwa wa Ngiri au Herina kwa kimombo ni matokeo ya kuwepo kwa udhaifu au kuwepo kwa uwazi katika tissue ambayo inashikilia viungo fulani katika mwili hivyo husababisha viungo hivo kutojishikilia vizuri katika sehemu inayostahili kuwwepo.

 Kuwepo kwa sehemu ya mwili ambayo inakuwa na udhaifu au tundu husababisha baadhi ya sehemu za ndani  za mwili  kuweza kujipenyeza na kutokea upande wa pili. Mara nyingi viungo vinavyoasiliwa sana ni sehemu za kokwa, tumbo, koradani n.k, Ambapo kwa sehemu ya mwili hupita katika matundu yanayopitisha mishipa ya fahamu(Spermatic cord) na hatimai kupatikana kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

Mshipa wa ngiri unaweza kutokea sehemu kama kinena,juu ya paja,sehemu za tumbo,kifua, na sehemu illiyowahi kufanyiwa upasuaji siku za nyuma.

AINA ZA NGIRI

  • Ngiri kavu, (Inguinal hernia)

  • Ngiri ya Tumbo(Abdomiana Hernia)

  • Ngiri ya kitovu(Umbilical hernia)

  • Ngiri ya sehemu ya haja kubwa(Anal henia)

  • Ngiri ya kwenye kifua (Hiatals hernia)

hiatal hernia

  • Incisiaonal hernia(Hutokea sehemu iliyowahi kufanyiwapasuaji kipindi cha nyuma)

incisional hernia

SABABU ZA HERNIA

Herina husababishwa kutokana na udahifu  na utumikaji wa tishu(misuli), kutegemeana na sababu zake herina huweza kukua ndani ya muda mfupi au mrefu.

Sababu kuu za udhaifu wa Tishu(misuli);

  • Umri
  • Kikohozi sugu(Cha muda mrefu)
  • jeraha kutokana na upasuaji
  • Congenital defect

Sabau zinazotokana na Utumikaji wa misuli ni;

  • kuwa mjamzito, hupelekea kuongezeka kwa pressuere katika tumbo
  • kupata choo kigumu kinachopelekea kutumika sana kwa misuli ya tumbo na Anal
  • kunyanyua vitu vizito
  • Kujaa kwa maji kwenye tissue za tumbo(Ascites)
  • Kuongezeka kwa uzito ndani ya muda mfupi
  • kukohoa  mara kwa mara
  • kufanyiwa upasuaji

DALILI ZA HERNIA

  • Kutokea na uvimbe(Lump katika sehemu iliyoathiriwa) unaweza kuitambua kwa urahisi wakati unapiga chafya au unainuka  kutoka kitako, au ukipinda. kwa mtoto utaitambua akiwa analia amabyo ni Hernia ya kitovu(Umbilical hernia).
  • Kujisikia maumivu katika sehemu iliyoathiriwa,mara nyingi maumivu sehemuu ya chini ya tumbo wakati wa kukohoa,chafya au kujipinda/kuinama
  • Kuhisi gas au ujazo ndani ya Tumbo.
  • kuhisi kichomi katika sehemu iliyovimba/baji

Dalilii zingine za hernia ya kifua/hiatal hernia ni;

  • Maumivu ya kifua
  • Maumivu wakati wa kumeza chakula 
  • Maumivu ya asidiki/muunguzo ambayo hutokea wakati asidi ya tumbo inarudi kwenye eosophagus

*****Baadhi ya hernia huwa azina dalili lakini unaweza kuzitambua   kutokana na uchuguziw a mara kwa mara*****

VIPIMO VYA KUITAMBUA HERNIA

Ngiri ya inguinal au incisional Daktari anaweza kuifahamu kwa kufanya uchunguzi wa  mwili wako ambako ataweza kuitambua baji,lump/ uvimbe katika sehemu iliyoathirika ambayo inaongezeka ukumbwa ukiwa unakohoa au kuinama.

Kwa mtu mwenye Ngiri ya kifua(Hiatal hernia) daktari anaweza kuitambua kwa kufanya kipimo cha Barrium X ray au endoscopy

MATIBABU

Matibabu ya hernia yanategemea ukumbwa na hatari ya dalili zake. Matibabu ya hernia yanaweza kuwa kwa kubadilisha mfumo wa maisha, dawa na upasuaji.

Kubadilisha mfumo wa maisha 

Daktari atakuelekeza ni aina gani ya mazoezi yanafaa kufanya, mazoezi haya yanaweza kusaidia misuli kuwa imara zaidi, lakini pia yakupasa kuwa makini kwa sababu kuna baadhi ya mazoezi yanaweza kuongeza msukumo katika eneo lililoasirika na matokeo yake kuongeza ukumbwa wa tatizo.

Kama mazoezi hayasaidii kuondoa/kupunguza Ngili, njia itaakayotumika ni upasuaji.

Kutumia dawa

kwa hernia ya kifua (Hiatal hernia) dawa zitatumika kuondoa mauzi/maumivu yanayosababishwa na asidi ya tumbo, dawa hizo zitapunguza kiwango cha asidi.

dawa hizo ni Antacid, H-2 receptor blockers,proton pump inhibitors

Upasuaji

Kama ngiri inakuwa kumbwa na kusababisha maumivu makali daktari ataamua njia ya upasuaji kwa kuwa ndio njia sahihi kwa muda huo.Laparascopic surgery ni upasuaji mdogo unaotumia camera ndogo sana(tiny camera) na vifaa vidogo vya upasuaji(miniaturised surgical equipment) ambavyo haviwezi kusababisha majeraha katika maeneo kuzunguka sehemu athirika.

Upasuaji mwingine ni open Sugery ambayo huwa inachukua muda mrefu paka kupona, makadirio ni paka week sita.

muhimu; Sio Mishipa ngirii yote inaitaji kufanyiwa upasuaji, kwa mfano ngiri inayotokana na kujiingiza kwa utombo katika Scrotum.

MATOKEO YA HERNIA KAMA HAIJTIBIWA

Kama mshipa ngiri haujatibiwa unaweza kukua zaidi na  kuzui mwenendo wa utumbo na kusababisha maumivu na kichefuchefu au kutokupata kwa choo kumbwaa(constipation). Pia inaweza sababisha kuongezeka kwa mkandamizo kwenye tishu za karibu na kusababisha kutokea kwa uvimbe na maumivu . 

Sehemu ya mshipa ngiri ikikosa oxygen kunatokea Strangulation ambayo ndio hatua mbaya zaidi ya Hernia inayoweza kumpelekea mgonjwa kifo.

Muhimu: Strangulated hernia ni hali ya dharula na inaitaji matibabu ya haraaka sana.