Kwanini wanaume wengine wanakua na matiti,je ni njia ipi ya kuondosha hayo matiti??
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha kukua kwa matiti isivyo kawaida kwa wanaume/wavulana lakini sabu zote zinatokana na kutowiana kwa hormones za Estrogen(for female traits) na testosterone (for male traits).
Hizi ni baadhi ya visababishi vya matiti makumbwa kwa wanaume(GYNOECOMASTIA) :
👉 Matumizi ya baadhi ya madawa(Medications) kama dawa zinazotumika kwa wanaoishi na virus vya ukimwi(EFAVIREZ), 💠Dawa zinzotumika kukuza misuli ambayo inatolewa na madaktar kwa makusudio maalumu(Wanariadha wanatumia kukuza misuli ambako ni kinyume na sheria) 💠Dawa zinazotumika kutibu Tenzi dume na baadhi ya vimbe za koradani, figo nk "💠Madawa ya kulevya kama Herroin, Marijuan na pombe. nk.
👉 Matatizo ya kiafya(Medical conditions)
kama:💠Hyperthyroidism >Kutokana na mabadiliko ya hormones, 💠Hypogonadism(Uzalishaji mdogo/kiwango kidogo cha testosterone hormones, 💠Kindney failure(Kufeli kufanya kazi kwa figo) >Athari itatokana na madawa yatakayotumika kutibia💠Uvimbe katika Tenzi(Tenzi dume) au korodani au Figo 💠nk
👉Mabadiliko ya ukuaji hasa Kipindi cha hatua za kubalekhe(Adolescent stage) na uzee => kwa vijana huwa hali hii inapotea ndani ya kipindi cha miezi 6 mpaka miaka 2.
👉 Baadhi ya watoto wachanga ni kutokana na kubeba estrogen hormones za mama=>inapotea nadani ya wiki 3 mpaka miez 3
👉 Utapia mlo(Malnutrition) =>Testosterone hormones zinapungua mtu akiwa na utapiamlo na estrogen zinabaki zikiwa sawa.
Gynaecomastia(Matiti makubwa kwa wanaume) Haina madhara makubwa kwa muathirika ingawaje inaweza sababisha matatizo ya saikolojia na hisia, na wakati mwingine maumivu ya matiti.
👉 💊 Matibabu yake ni kwa kutumia dawa za kusawazisha hormones(Hormonal Therapy) au Surgery (Upasuaji)
Muhimu:👉 Ni vizuri kumuona daktari unapohisi maumivu, kuchuja kwa matiti(majimaji au usaha) uvimbe.
👉Ni vizuri kumuuliza daktari juu ya dawa unazotumia kama zinaweza sababisha matiti makumbwa