njia gani sahihi ya kuzuia mimba na haina madhara kwa mtumiaji?
JIBU;
Tufahamu kuwa njia za uzui wa mpango ambazo zimeainishwa katika muongozo wa taifa zote ziko salama kwa mtumiaji, Ingawa kuna maudhi makubwa au badogo ambayo yanaweza kutokea kwa mtumiaji , Jambo la muhimu katika kufanya maamuzi ya ipi ni njia sahihi ni kwa kuangalia malengo yako,hali yako ya kiafya ,mashauri na Mpenzi wako,pamoja na ushauri wa wataalamu wa Afya.
Baadhi ya mambo unayotakiwa kuangalia katika kuchagua njia ya Sahihi ya uzazi wa mpango ni;
- Ina ufanisi kiasi gani katika kuzuia mimba?.
- Ina ufanisi kiasi gani katika kukinga dhidi ya magonjwa ya ngono?.
- Kama mwenzi wako anaafiki matumizi ya njia hiyo ya uzazi wa mpango, au kama unapaswa kuficha asijue.
- Kama njia hiyo inapatikana kwa urahisi, na mara ngapi unatakiwa kiutumia katika muda fulani
- Inagharimu kiasi gani ?.
- Kama ina madhara ya pembeni.
- Kama una mahitaji na wasi-wasi mwingine. Kwa mfano: unanyonyesha? Bado unahitaji watoto zaidi ?
NJIA YA UZAZI WA MPANGO | Uwezo wa kuzuia mimba | Uwezo wa kukinga dhidi ya maambukizi kupitia ngono | Matumizi yake | Maelezo mengine muhimu |
---|---|---|---|---|
Kondom | Mkubwa | Mkubwa zaidi | Wakati wote | Hufanya kazi kwa ufanisi zaidi inapotumika na dawa ya kuua mbegu za kiume na kilainishi cha asili ya maji. Kondom hutakiwa kutumika kila mara unapofanya tendo la ngono. |
Vidonge vya majira-Vidonge mseto | Mkubwa sana | Sifuri | Kila siku | Hufanya kazi vizuri zaidi inapotumika muda ule ule kila siku. Wanawake wenye matatizo ya kiafya yafuatayo hawapaswi kutumia njia hii. |
Vidonge vya majira (vyenye homoni moja-siyo mseto) | Mkubwa sana | Sifuri | Kila siku | Hufanya kazi pale tu inapotumiwa saa ile ile kila siku. Inaweza kutumiwa hata na wanawake wanaonyonyesha (anza angalau baada ya mtoto kufikisha wiki 6). |
Vijiti | Mkubwa zaidi | Sifuri | Miaka 3 hadi 5 | Lazima vingizwe na kutolewa na mfanyakazi wa afya ambaye amepitia mafunzo maalum na kubadilishwa kila baada ya miaka 3 au 5 kutegemea na aina ya vijiti. |
Sindano | Mkubwa sana | Sifuri | Mwezi 1, 2, au 3 | Inatakiwa kurudiwa kila baada ya mwezi 1, 2, au 3 (kutegemea na aina ya sindano). |
Kitanzi | Mkubwa zaidi | Sifuri | Miaka 5 au 12 | Hufanya kazi kwa muda wa miaka 5 au 12 (kutegemea na aina ). Lazima kiingizwe na kutolewa na mfanyakazi wa afya ambaye amepitia maafunzo maalum. |
Kuchomoa uume mwanaume anapofikia kileleni | Mdogo sana | Sifuri | Wakati wote | Mwanaume anatakiwa kuchomoa uume wake haraka anapofika kileleni kila mara mnapofanya tendo la ngono. Hata kama atachomoa uume, majimaji kidogo kutoka umeni yanaweza kuingia ukeni wakati wa tendo la ngono na kusababisha mimba kutunga, hali ambayo pia inaweza kusababisha maambukizi yanayopitia ngono. |
Unyonyeshaji (wakati wakati wa miezi miezi 6 tu ya kwanza) | Mkubwa sana | Sifuri | Mara kadhaa mchana na usiku | Njia hii hufanya kazi tu kama mwanamke ananyonyesha mtoto wake maziwa ya mama tu na kama hedhi zake hazijaanza tena. |
Njia ya kuhesabu siku (kushika mimba) | Mkubwa | Sifuri | Kila mara | Njia hii haifanyi kazi vizuri kwa wanawake wenye mzunguko wa hedhi unaobadilika. |
Tendo la ngono lisilohusisha uume kuingizwa kwenye uke | Mkubwa zaidi | Inategemea | Kila mara | Kama uume haugusi uke, mwanamke hawezi kupata mimba. Ngono kwa njia ya haja kubwa inaweza kusababisha maambukizi kwa urahisi. Ngono kwa njia ya mdomo ina uwezekano mdogo wa kusababisha maambukizi ya magonjwa yanayopitia ngono. Mguso tu wa kingono bila kuingiliana ni nadra kusababisha maambukizi yoyote. |
Kufunga kizazi kabisa | Mkubwa zaidi | Sifuri | Mara moja | Mara mwanamke au mwanaume anapofunga kizazi kabisa, hatabeba mimba au kusababisha mimba tena. |
Watu wengi huchagua njia za uzazi wa mpango kutokana na mazingira yao.mfano;
- binti hataki wazazi wake wafahamu kama anatumia njia za uzazi wa mpango,
- Mtumishi ataki kuzaa paka kufikia miaka kadhaa
- wapenzi wasiofunga ndoa na hawataki kupata mtoto kabla ya ndoa
- Mwanafunzi hataki kuaribu masomo yake kwa ajili ya mimba