UGONJWA WA MATUMBO(Typhoud)
Ugonjwa wa matumbo(Typhoid)
Homa ya matumbo (kwa Kiingereza typhoid fever) husababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella Typhi. Ugonjwa huu huambukizwa kwa mtukula au kunywa chakula au maji yaliyo na kinyesi cha mtu aliyambukizwa. Bakteria hawa hutoboa na kunyonya chakula kwenye matumbo ya binadamu
Dalili za Typhoid
- Homa kali
- Kutoka kwa jasho jingi
- Kuharisha (bila ya kutoa damu)
- Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.
Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.
Katika wiki ya kwanza:
- Joto la mwili huongezeka
- Kichwa huuma
- Kukohoa
- Damu kutoka puani, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
- Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea
Katika wiki ya pili:
- Homa huongezeka
- Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
- Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
- Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
- Kutapika kwa mgonjwa
- Ini la mgonjwa huvimba
- Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.
Wiki ya tatu:
- Matumbo hutoa damu.
- Matumbo hutoboka
- Wiki ya tatu ikimalizika, homa huanza`kutulia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.
Matibabu
Mara nyingi, homa ya matumbo haiui binadamu. Dawa kama ampicillin, chloramphenicol, trimethoprim-sulfamethoxazole, amoxicillin and ciprofloxacin hutumika kutibu ugonjwa wa matumbo.
Hatua za kuzuia kupata homa hii
- Usafi wa mazingira na wa kinafsi ni hatua bora ya kujikinga kutokana na ugonjwa huu.
- Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hiyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
- Homa hii huweza kuenea kwenye mazingira ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao.
- Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kingo bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
- Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majina Typhim Vi iliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherix iliyotengenezwa na GlaxoSmithKline.