Mimba inaweza kuonekana kwenye kipimo baada ya siku ngapi? na dalili kwa mtu mwenye mimba ni zipi?
JIBU:
Kwanza kabisa tufahamu kuwa mizunguko ya hedhi kwa wanawake inatofautiana,kuna baadhi wanaenda siku nyingi na wengine chache(kwa makadirio ya siku (3-7).
Yai la mwanamke linapokutana na mbegu za mwanaume huwa inachukuaa siku 7-10 kujishikiza katika ukuta wa mfuko wa kizazi na kisha uchukua siku 2-3 mimba kuweza kusomwa katika kipimo, Hivo basi kwa makadirio mimba inawweza kuonekana siku 14-21 baada ya kukutana na mwanaume.
pia baadhi ya urine strips(UPT) inaweza onyesha kuanzia siku 7.
Dalili za mimba.
Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwanamke mwingine, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana ya ujauzito.
dalili na ishara za ujauzito:
- Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii
- Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa ya ujauzito
- Maumivu kwenye matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)
- Uchovu, wanawake wengi huhisi uchovu na na hali ya kutopenda kufanya lolote.
- Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni
- Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu
- Kichefuchefu na kutapika
- Maumivu ya kichwa
- Kizunguzungu
- Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)
- Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi
- Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine
- Kupanuka kwa mfuko wa uzazi
- Tumbo kujaa au kuvimbiwa
- Kununa na kukasirika haraka
- Kiungulia au kupata choo kigumu
- Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti
- Kuongezeka uzito
- Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)
- Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6
- Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii hujulikana kama Chadwick's sign
Dalili nyingine ni pamoja na
- Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)
- Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)
- Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.
- Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).
- Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto
- Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound