KWA NINI MWANAMKE ANAYETUMIA DEPOVERA(sindano) KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO KWA ZAIDI YA MARA 3 HUWA ANACHELEWA KUPATA MIMBA?



Ahsante kwa kuwa mtumiaji wa Afya yangu app, Majibu  ya swali lako ni kama ifuatavyo:

 

Ni kweli kwa mwanamke ambaye anatumia njia ya uzazi wa mpango aina ya Depovera huwa wanachelewa kupata mimba mara baada ya kuaacha kutumia kwa nji hiyo ambayo kwa makadirio anaweza chelewa kwa miezi sita au zaidi na kwa baadhi ya wanawake wanafika mpaka mwaka 1 au 2.

Kutokana na hili ndio maana inashauriwa kuwa kwa mwenye matarajio ya kupata mimba karibuni sio vema kutumia njiaa hii ya uzazi wa mpango.

Sindano ya depovera kawaida huwa inachomwa kila baada ya miezi 3 na asili yake ni hormone ya projestini ambayo kazi yake kuifanya mirija ya fallopian kuwa na ukavu kiasi cha mbegu za kiume(sperms) kushindwa kusafiri katika mirija kufika katika yai la mwanamke kwa ajili ya uchevushaji. Kutokana na hili kwa baadhi ya wanawake huwa inakaa muda  mrefu zaidi, kwa makadirio ya miezi 6 mpaka miaka 2 kisha hurudi katika hali yake ya kawaida na kuweza kushika mimba tena.

Depo provera can cause temporaly infertillity?             "YES"