DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO NI IPI? NIFANYE NINI ILI KUPUNGUZA ASIDI TUMBONI?



Ahsante kwa kuwa mtumiaji wa Afya yangu App, Majibu ya swali lako ni kama ifuatavyo;

 

Matibabu ya Vidonda vya tumbo(PUD) inategemeana na chanzo au sababu ya tatizo hilo, ambapo kunaweza kuhusishwa kwa kuondoa kwa bacteria aina ya H.pyolori, kupunguza au kuacha matumizi ya Non Storoids Antinfalamatory Drug(NSAIDS)  sambamba na kutumia dawa zitakazo ponya vidonda.

Matumizi ya dawa za Antibiotics kwa ajili ya kuondoa H.pylori

Mganga wako atakupatia mjumuiko wa dawa amabzo zitatumika katika kuondoa wadudu aina ya H.pylori, miongoni mwa dawa hizo ni; amoxicillin (Amoxil), clarithromycin (Biaxin), metronidazole (Flagyl), tinidazole (Tindamax), tetracycline (Tetracycline HCL) and levofloxacin (Levaquin).

Daktari atakupatia dawa kulingana na sehemu unayoishi na pia kuangalia hali ya usugu wa dawa kwa wadudu pia anaweza kukuongezea dawa zingine kwa ajili ya kupunguz kiwango cha asidi ya  tumbo,  dawa jamii ya Proton pump inhibitol    mfano..bismuth subsalicylate (Pepto-Bismol)

Dawa inayozuia kuzalishwa kwa asidi na kuponya vidonda

Dawa aina ya PPI au Proton Pump Inhibitors huzuia kuzalishwa kwa asidi katika tumbo kwa kuzuia sehemu za seli zinazohusika na uzalishaji wa asidi. Dawa zinazotumika ni kama omeprazole (Prilosec), lansoprazole (Prevacid), rabeprazole (Aciphex), esomeprazole (Nexium) and pantoprazole (Protonix).

Tahadahari; Matumizi ya muda mrefu na hasa kwa dozi kumbwa ya dawa za PPIs kunaweza kuongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa ya wrist,hip na spine. Kutokana na hilo Daktari anaweza akakupatia pia dawa za Vitamins(Vitamini Supplements) kwa ajili ya kupunguza hatari ya kupata tatizo hilo.

Dawa za kupunguza uzalishaji wa asidi ya tumbo

Dawa aina ya Acid Blochers au kwa jina la histamines(h-2) Blockers Hupunguza kuzalishwa kwa asidi tumboni hivyo kupunguza maumivu ya tumbo na kuchochea kupona kwa vidonda. Dawa hizo ni kama ranitidine (Zantac), famotidine (Pepcid), cimetidine (Tagamet HB) and nizatidine (Axid AR).

Dawa inayolinda kuta za tumbo na utumbo mdogo

Kulingana na hali yako daktaria anaweza akakupatia dawa aina ya cytoprotective agents kwa ajili ya kulinda tishu zilizopo katika kuta za tumbo na utumbo mdogo, dawa;sucralfate (Carafate) and misoprostol (Cytotec). 

ZINGATIA: Matumizi ya dawa ni baada ya ushauri wa daktari

Nifanye nini ili kupunguza asidi ya tumbo?

  • Matumizi ya matunda yaliyo na Vitamins A na C  na mbogamboga, Epuka vyakula vyenye vitamins nyingi zaid, hii itasababisha kuchelewa kwa kupona kwa vidonda.
  • Tumia vyakula vyenye Probiotics, kama vile Yogut na Miso
  • Punguza msongo wa mawazo , hii inaweza kuwa ngumu baadhi ya wakati lakini jitahidi kukubaliana na mazingira halisi
  • Acha au punguza matumizi ya pombe
  • Pata muda wa kutosha wa kulala, Itasaidia kupunguza msongo wa mawazo na pia kuboresha kinga yako ya mwili . Epuka kula muda mfupi kabla ya kwenda kulala